Loading...

Wizi wa Tanzanite waishtua Serikali.




Arusha. Serikali imeanza kuifanyia uchunguzi Kampuni ya Crown Lapidey kwa kuiandikia barua ijieleze baada ya Mahakama ya Mkoa Kilimanjaro kuitaja kuhusika kula njama na mfanyabiashara raia wa India, Anarag Jain (44) kutorosha Tanzanite. 

Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane alisema jana kuwa, uchunguzi huo wanafanya kwa kushirikiana na wanasheria. Jain aliyekamatwa mwaka jana na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kutorosha madini hayo yenye thamani ya Dola 310,137 za Marekani.


ZeroDegree.
Wizi wa Tanzanite waishtua Serikali. Wizi wa Tanzanite waishtua Serikali. Reviewed by Zero Degree on 1/20/2016 07:53:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.