Loading...

CHAMA CHA MAPINDUZI [ CCM ] kimelaani vikali kitendo cha nyumba za wafuasi wake kupigwa alama ya X.


CHAMA CHA MAPINDUZI kimelaani vikali kitendo cha kuwekwa alama ya X kwenye nyumba za wafuasi wake Kisiwani Pemba.

Pia CCM imesikitishwa na kulaani vikali kitendo cha kuchoma moto tawi la CCM la Kengeja.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Bi Waride Bakari Jabu akizungumza na wanahabari ofisini kwake Kisiwandui amesema kitendo cha kuchoma moto ofisi za CCM na kuweka X nyumba za wafuasi wa CCM maeneo ya Mtambile, Kengeja, Minazini, na Kangani katika Wilaya ya Mkoani kuna lengo la kuvunja Amani na Usalama visiwani humo.

CCM imetoa wito kwa wazanzibar hasa wafuasi wa CCM kupuuza vitendo hivyo na kutolipa kisasi na badala yake waelekeze nguvu katika maandalizi ya uchaguzi wa marudio uliotangazwa kufanyika Machi 20.

Lakini pia CCM inatoa wito kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha kuwa wanafanya kazi yao kwa umakini zaidi ili kuzuia uhalifu na njama za kuvuruga amani Visiwani, Zanzibar.



ZeroDegree.
CHAMA CHA MAPINDUZI [ CCM ] kimelaani vikali kitendo cha nyumba za wafuasi wake kupigwa alama ya X. CHAMA CHA MAPINDUZI [ CCM ] kimelaani vikali kitendo cha nyumba za wafuasi wake kupigwa alama ya X. Reviewed by Zero Degree on 2/13/2016 12:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.