Serikali kujenga Nyumba 3500 kwa Ajili ya askari Polisi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Masauni Yusufu Masauniameyasema hayo leo mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduma Mheshimiwa Frank Mwakajoka aliyetaka ufafanuzi wa lini serikali itaboresha na kuongeza nyumba za askari polisi nchini.
Naibu Waziri Masauni amesema kuwa ni dhamira ya serikali kuhakikisha jeshi la polisi linaboresha makazi na kuwa na ofisi ili kuwezesha utoaji wa huduma kwa wananchi kuwa mzuri na pindi mkopo huo utakapo kamilika ujenzi utaanza kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa kwa sasa wapo katika mpango wa awali wa kujenga nyumba 350 nchi nzima ambazo zitatatua tatizo hilo la walinzi wa raia na mali za wa Tanzania kukosa makazi bora na ya kudumu.
ZeroDegree.
Serikali kujenga Nyumba 3500 kwa Ajili ya askari Polisi.
Reviewed by Zero Degree
on
2/01/2016 06:46:00 PM
Rating: