Loading...

SHEHENA ya madawa ya kulevya kutoka Kenya yakamatwa mpakani



Shehena ya bidhaa aina ya mafuta ya Taa na dawa za kulevya kilo 98 zilizokuwa zikiingizwa nchini kwa njia za panya kutoka nchini Kenya zimekamatwa katika mapori yanayounganisha mpaka wa nchi jirani, katika operesheni maalum inayofanywa katika vijiji tofauti vilivyopo mpakani ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na mtandao wa kihalifu unaojihusiosha na uingizaji wa dawa za kulevya, wahamiaji haramu na ukwepeji wa kodi kwa serikali.

Wakizungumza katika eneo la Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania timu ya watendaji wa mamlaka ya mapato nchini (TRA), maafisa uhamiaji na wakaguzi wa mamlaka ya chakula na dawa nchini tawi la Horohoro, wamesema lengo la operesheni hiyo ni kuhakikisha kuwa mipaka ya nchi inakuwa salama kufuatia kubainika kuwepo kwa mtandao wa ukwepaji kodi, kupitisha wahamiaji haramu na vikundi vya uhalifu.

Kuhusu kukamatwa kwa dawa za kulevya mratibu mwandamizi msaidizi wa idara ya uhamiaji nchini tawi la Horohoro Mwesiga Lubalila amesema katika zoezi la kukabiliana na uingizaji wa bidhaa haramu, kundi la watu waliokuwa na pikipiki zilizokuwa zimebeba maboksi walipobaini mtego wa kukamatwa walilazimika kuzitupa pikipiki hizo na kisha kukimbia ndipo walipopekua na kukuta dawa za kulevya aina ya Mirungi kilo zenye uzito wa kilo 98 iliyokuwa imefungwa katika vifurushi vyenye uzito wa kilo mojamoja kila kimoja.

Kufuatia hatua hiyo mkaguzi mkuu wa mamlaka ya chakula na dawa Bwana Thomas Nkondola amesema bidhaa zote zinazoingizwa kutoka nchini Kenya hazitaruhusiwa kuingia endapo kama hazijafanyiwa ukaguzi kufuatia baadhi ya wafanyabiashara kuingiza bidhaa zilizopitwa muda wake na hivyo kuhatarisha afya za watumiaji.




ZeroDegree.
SHEHENA ya madawa ya kulevya kutoka Kenya yakamatwa mpakani SHEHENA ya madawa ya kulevya kutoka Kenya yakamatwa mpakani Reviewed by Zero Degree on 2/17/2016 09:24:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.