Loading...

Vijana wahimizwa kubeba kondomu siku ya wapendanao.


Bangkok, Thailand. Wahenga walivyosema kuwa duniani kuna mambo na mengi ya hayo. Hivyo ndivyo inavyodhihirika hasa wakati huu ambapo dunia ikijiandaa kusherekea siku ya wapendanao ya Valentine.

Hivyo, Serikali ya Thailand imezindua kampeni kabla ya siku ya wapendanao ya Valentine ikiwataka vijana nchini humo kutosikia aibu wanapobeba mipira ya kondomu.

Mpango huo unaonekana kubadilika ikilinganishwa na kampeni zilizokuwa zikifanywa hapo awali na vijana walihamasishwa kuzuru maeneo ya kidini na baadaye kwenda nyumbani baada ya mikutano na wapenzi wao badala ya kujihusisha na ngono.

Thailand ina idadi kubwa ya wasichana waliopata mimba duniani pamoja na viwango vya juu vya magonjwa yanayoambukizwa kupitia ngono.

Kampeni hiyo inayotarajiwa kuendelea hadi mwaka 2019, inaambatana na mipango ya hivi karibuni inayolenga kuangazia mimba za wanafunzi.

Mamlaka nchini humo zimekuwa zikihamasisha umuhimu wa kutumia mipira ya kondomu pamoja na kuwashauri vijana kutoshiriki ngono.

Wakati mkakati huo ulikuwa ukitekelezwa zaidi katika miaka ya nyuma, Serikali imekuja na mkakati mpya ikiwalenga vijana kuwa na mwamko wa utumiaji wa kondomu.

Kampeni hiyo ambayo pia inaungwa mkono na taasisi za kiraia, imekusudia kukabiliana na tatizo la unyanyapaa kuhusu matumizi ya mipira ya kondomu pamoja na kurahisisha upatikanaji wake.

Msemaji wa Wizara ya Afya nchini Thailand, Lertwi Lairrattanapong amesema kuwa vijana wanapaswa kuacha aibu kuhusu ununuzi wa mipira ya kondomu.

‘’Jamii pia inafaa kukubali kwamba wasichana wanapaswa kutumia kondomu kwa ajili ya kujinga na siyo kuendelea kusubiri wakipata mimba,” alisema ofisa huyo. Siku ya wapendanayo huadhimishwa kila mwaka Februari 14.



ZeroDegree.
Vijana wahimizwa kubeba kondomu siku ya wapendanao. Vijana wahimizwa kubeba kondomu siku ya wapendanao. Reviewed by Zero Degree on 2/06/2016 12:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.