Loading...

Kipindupindu chashika kasi Tarime


Tarime. Watu wawili wamepoteza maisha na wengine 15 kulazwa Kituo cha Afya Nyamongo wilayani hapa, baada ya kuugua kipindupindu kwa kutozingatia usafi na ukosefu wa vyoo.

Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Tarime juzi, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorias Luoga alisema ugonjwa huo upo katika Kata ya Nyamongo.

Luoga alisema kata hiyo ina maeneo ya machimbo na shughuli nyingi za mamalishe na kwamba, baadhi ya watu hawazingatii usafi na hakuna vyoo, hali inayosababisha kujisaidia eneo lolote.

“Nyamongo bado kipindupindu kipo wamekufa wawili, 10 wamelazwa na watano wameruhusiwa. Nawaomba zingatieni usafi kwenye nyumba zenu na maeneo ya vyakula, mamalishe hakikisheni vyakula vinakuwa vya moto, chemsha maji ya kunywa maana Tarime hatuna maji salama,” alisema Luoga.

Baadhi ya wananchi walisema Serikali imekuwa ikiwahamasisha kufanya usafi, lakini masoko yamekithiri kutokana na takataka kutozolewa kwa wakati.

Mkazi wa Turwa, Charles William alimwambia Luoga kuwa kuna jalala karibu na Soko la Reb, eneo ambalo watu wanauza bidhaa na vyakula.

Pia, alimweleza kuwa hata eneo alipokuwa akihutubia mkutano hakuna choo wala mahali pa kujisaidia haja ndogo.

Luoga alisema siyo sahihi jalala kuwa karibu na soko na aliagiza uongozi wa halmashauri ya mji kuhamisha takataka zilizopo katika soko hilo.



ZeroDegree.
Kipindupindu chashika kasi Tarime Kipindupindu chashika kasi Tarime Reviewed by Zero Degree on 2/06/2016 12:09:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.