Loading...

Huu hapa mkakati wa BUNGE la Tanzania na Vietnam.


SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amesema Bunge la Tanzania litaendelea kuimarisha na kukuza ushirikiano na Bunge la Vietnam, ikiwa ni muendelezo wa uhusiano nzuri ulipo baina ya mataifa hayo mawili.

Ndugai aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi habari, muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Vietnam Troung Tang Sang anayeondoka nchini leo, baada ya kumaliza ziara yake ya siku nne hapa nchini.


Mhe ,Job Ndugai

Alisema Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Vietnam kwa muda mrefu na kwamba mwaka 2009 wabunge wa Tanzania walitembelea Bunge la Vietnam. Pia mwaka 2011 wabunge wa nchi hiyo nao walitembelea Bunge la Tanzania na kufanikiwa kubadilisha uzoefu wa mabunge yao.

Ndugai alisema kupitia uongozi wake atahakikisha uhusiano unakuwa endelevu kwa faida ya nchi na Watanzania wote. “Rais wa Vietnam na mimi tumekubaliana kushirikiana katika masuala mbalimbali ya Bunge, ukuzaji uchumi na biashara na kuimarisha uhusiano wa mabunge yetu zaidi,” alisema.

Katika mazungumzo, Ndugai aliongozana na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti Hawa Ghasia, Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji na Mbunge wa Segerea Bonnah Kalua ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje. Leo Rais huyo anaondoka nchini kwenda Msumbiji kwa ziara ya kikazi.




ZeroDegree.
Huu hapa mkakati wa BUNGE la Tanzania na Vietnam. Huu hapa mkakati wa BUNGE la Tanzania na Vietnam. Reviewed by Zero Degree on 3/11/2016 08:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.