Loading...

Soma AGIZO la waziri wa kilimo, uvuvi na mifugo juu ya VOCHA ZA PEMBEJEO.


Serikali ya Tanzania imewaagiza mawakala wa Pembejeo za kilimo nchini kuhakikisha kuwa wanawafikishia wakulima vocha za pembejeo za kilimo kwa wakati ili waweze kuzalisha chakula kwa wingi na nchi kuwa na uhakika wa chakula.

Agizo hilo limetolewa na waziri wa kilimo, uvuvi na mifugo Mwigulu Nchemba kufuatia malalamiko ya wakulima wilayani Rungwe mkoani Mbeya ya kucheleweshewa pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea hali inayopelekea kuzalisha chakula kidogo tofauti na matarajio.

Kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wakulima dhidi ya mawakala wa Pembejeo za kilimo mkoani Mbeya ya kupewa Vocha za Mbejeo baada ya msimu kuanza hali inayopekea wakulima hao kuhisi watendaji na mawakala wana nia ya kuhodhi pembejeo hizo.

Waziri Nchemba amesema wakulima wanahitaji kuzalisha kisasa kwa kuzalisha chakula kwa wingi kwa kutumia mashamba madogo na kuwa Serikali itahakikisha inawapatia mbegu bora ili kutimiza adhma hiyo.




ZeroDegree.
Soma AGIZO la waziri wa kilimo, uvuvi na mifugo juu ya VOCHA ZA PEMBEJEO. Soma AGIZO la waziri wa kilimo, uvuvi na mifugo juu ya VOCHA ZA PEMBEJEO. Reviewed by Zero Degree on 3/13/2016 10:39:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.