Dr Shein atangaza baraza lake la mawaziri, soma hapa majina yaliyounda baraza hilo.
RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein leo Jumamosi, April 9, 2016 ametangaza Baraza la Mawaziri litakalosimamia kazi za serikali kwa kipindi cha uongozi wake wake kwa mujibu wa sheria.
Dkt. Shein amesema amepunguza ukubwa wa baraza hilo kutoka wizara 16 hadi kuwa wizara 13, ambapo wizara tatu amezivunja na kuzigawa ndani ya hizo wizara 13 za sasa. Mawaziri ni 13 na Manaibu waziri 7.
Ameongeza kuwa, mawaziri aliowatangaza leo atawaapisha kesho Jumapili asubuhi katika Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar.
Baraza hilo la Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni:-
- Waziri Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi – Issa Haji Ussi Gavu
- Waziri wa Katiba na Sheria Utumishi wa Umma -Haroun Ali Sleiman
- Waziri wa Tawala za Mikoa na Idara Maalum-Hali Omari Kheir
- Waziri wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais- Mohd Aboud
- Waziri wa Fedha na Mipango-Dr Khalid Salum Mohd
- Waziri wa Afya-Mahmoud Thabit Kombo
- Wizara ya Elimu - Riziki Pembe Juma
- Waziri wa Viwanda na Masoko-Amina Salum Ali
- Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi -Ali Karume
- Wizara ya Habari, utalii, Utamaduni na Michezo -Rashid Ali Juma
- Wizara ya Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto- Maulidine Castiko
- Wizara ya kilimo, Maliasili na Uvuvi-Hamad Rashid Mohd
- Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Mazingira-Salama Aboud Talib
Jiunge nasi
ZeroDegree.
Dr Shein atangaza baraza lake la mawaziri, soma hapa majina yaliyounda baraza hilo.
Reviewed by Zero Degree
on
4/09/2016 05:14:00 PM
Rating: