Loading...

Kamera za VYOMBO VYA HABARI ndani ya BUNGE zapigwa marufuku.


BUNGE linaanza rasmi usajili wa wabunge na watumishi wa Bunge hilo pamoja na wageni mbalimbali, wanaoingia bungeni kwa kutumia mfumo wa kisasa wa kuchukua alama za vidole.

Sambamba na mfumo huo, Bunge pia limetoa taarifa rasmi ya kudhibiti urushaji wa matangazo ya Bunge ambayo sasa vyombo vya habari vya kielektroniki havitaruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa bunge na kamera kwa lengo la kurekodi yanayoendelea.

Na badala yake, jukumu la kurusha matangazo ya vikao vya Bunge litafanywa na Bunge lenyewe kupitia Feed Maalum ili kurahisisha kila kituo cha redio na televisheni kupata matangazo hayo kwa sehemu walipo bila kufunga mitambo yao bungeni.

Hayo yalibainishwa jana na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah wakati akitoa taarifa kwa Naibu Spika wa Bunge hilo, Dk Tulia Ackson alipofanya ukaguzi wa ukarabati uliofanywa ndani ya Ukumbi wa Bunge linaloanza vikao vyake vya Bajeti katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la 11 mjini hapa.

Dk Kashilillah alisema kuanzia jana wabunge wataanza usajili kwa njia ya kuchukuliwa alama za vidole badala ya utaratibu wa zamani wa kujisajili kwa kutumia makaratasi. 

Alisema usajili huo utachukua alama za vidole vyote 10 na lengo la kutumia mfumo huo ni kuboresha kanzi data ya Bunge na kwamba usaili huo utapunguza pia matumizi ya makaratasi ambayo yana gharama.

“Tumeanza usajili huo leo (jana) kwa wabunge waliofika, ila tutaendelea kusajili nadhani ndani ya wiki tutakuwa tumekamilisha kazi hiyo, na tumejipanga kuifanikisha kwa haraka,” alisema Dk Kashilillah.




ZeroDegree.
Kamera za VYOMBO VYA HABARI ndani ya BUNGE zapigwa marufuku. Kamera za VYOMBO VYA HABARI ndani ya BUNGE zapigwa marufuku. Reviewed by Zero Degree on 4/19/2016 04:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.