Hatma ya Rais Jacob Zuma kujulikana leo hii.
Spika wa Bunge hilo, Baleka Mbete alitoa taarifa hiyo baada ya shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani vikiongozwa na kile cha Economic Freedom Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema.
Mahakama ya Katiba nchini humo ilibaini kwamba Zuma alikataa kutii agizo kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu mwaka 2014 la kumtaka alipe kiasi hicho cha fedha.
Wakati Zuma akikubali kutii uamuzi wa Mahakama ya Katiba uliomtaka alipe fedha hizo za umma ndani ya miezi mitatu, upinzani umeanzisha ajenda inayotaka kiongozi huyo aondolewe madarakani.
Mahakama ya juu ya nchi juzi ilisema rais huyo alikiuka katiba ya nchi alipokataa kulipa fedha hizo alizozitumia kwa manufaa yake binafsi.
Katika hotuba yake Rais Zuma alisema ataiheshimu hukumu hiyo na ataitekeleza.
Hata hivyo, Rais Zuma ameupuuza wito wa upinzani unaomtaka ajiuzulu.
Wakati akipewa miezi mitatu kulipa deni hilo, alisema hukumu hiyo ya mahakama ni ishara ya kuwapo kwa demokrasia Afrika Kusini. Pia, alikanusha madai ya rushwa na udanganyifu.
Chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Democratic Alliance kilitaka rais huyo mwenye umri wa miaka 73 afunguliwe mashtaka.
Kuna uwezekano mkubwa wa pendekezo hilo kupingwa litakapowasilishwa leo katika bunge hilo linalodhibitiwa na chama cha Rais Zuma cha ANC.
Chama hicho cha upinzani kilitaka kuchukuliwa hatua nje ya Bunge za kumlazimisha Rais Zuma kujiuzulu.
Mkuu wa chama hicho, Mmusi Maimane alimewaambia waandishi wa habari kuwa Rais Zuma anapaswa kuondolewa madarakani haraka iwezekanavyo.
“Hukumu ya Mahakama ya Katiba iko wazi, Rais Zuma amevunja katiba. Ningelikuwa mimi, ningelianza mapema kuandika barua ya kujiuzulu,” alisema kiongozi huyo.
Zuma ni nani
Jacob Gedleyihlekisa Zuma alizaliwa Aprili 12, 1942 ni Rais wa Afrika Kusini tangu 2009.
Alikuwa makamu wa rais chini ya Thabo Mbeki kati ya 1999 na 2005. Tangu Desemba 2007 ni mwenyekiti wa chama tawala cha ANC.
Alizaliwa kama mtoto wa wazazi maskini katika eneo la Kwazulu-Natal. Akiwa na umri wa miaka 17 alijiunga na ANC akaingia katika upinzani mkali dhidi ya Serikali ya ubaguzi wa rangi wa kisheria.
1963 alikamatwa na kufungwa jela miaka 10 huko Robben Island pamoja na Nelson Mandela. Baada ya kutoka gerezani akaondoka Afrika ya Kusini na kushiriki katika shughuli za nje za ANC nchini Msumbiji na Zambia.
Nyumba ya Zuma.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF) Julius Malema alitekwa juzi usiku katika barabara ya Johannesburg.
Taarifa ambazo zilizopatikana kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kutoka kwenye chama hicho zilisema kwamba Kamanda huyo aliviziwa na takriban magari kumi ya polisi ambao wote walimelekezea mtutu wa bunduki baada ya kulizuia gari lake katika makutano ya barabara ya Grayston .
ZeroDegree.
Hatma ya Rais Jacob Zuma kujulikana leo hii.
Reviewed by Zero Degree
on
4/05/2016 02:01:00 PM
Rating: