Loading...

TANESCO yasamehe jumla ya shilingi bilioni 69 kwa Watanzania.


KUSHUKA kwa bei ya umeme kwa wateja wa kada mbalimbali wa nishati hiyo na kuondolewa kwa tozo ya huduma ya kila mwezi ya Sh 5,520 kwa kila mteja wa nyumbani, kumerudisha kwa Watanzania zaidi ya Sh bilioni 69, iliyokuwa ikienda katika Shirika la Umeme (Tanesco).



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi, amesema hayo mwishoni mwa wiki, alipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC).

Kwa mujibu wa Ngamlagosi, kufutwa tu kwa tozo ya kila mwezi ya huduma kwa wateja wa majumbani ambayo ilikuwa Sh 5,520, ambayo ni mbali na punguzo la bei kwa kada mbalimbali za wateja, kumewarejeshea Watanzania Sh bilioni 69, ambazo hapo awali zilikuwa zikienda Tanesco.

Alipoulizwa iwapo hatua hiyo ya kupunguza bei ya umeme imetokana na shinikizo kutoka serikalini na kama kutayumbisha shirika hilo muhimu kwa uchumi wa nchi. Ngamlagosi alisema, kwanza maombi ya kushusha bei hiyo yametoka Tanesco.

“Sisi tumepokea barua kutoka Tanesco ikituomba suala la kushusha bei ya umeme na sio kwamba walilazimishwa na Serikali na sisi tuliwahoji sana, kama wataweza kujiendesha, baada ya kuridhika na maelezo yao na uchunguzi wetu, ndipo tukakubali,” alisema Ngamlagosi.

Faida ya gesi Akifafanua matokeo ya uchunguzi uliochangia wakubali kushushwa kwa bei hiyo, Ngamlagosi alisema walibaini ukweli kwamba hivi sasa mitambo ya kuzalisha umeme huo unaouzwa na Tanesco, mingi haitumii tena mafuta, bali inatumia gesi asilia inayochimbwa hapa nchini.


Umeme wa mafuta ulikuwa ghali kwa kuwa kwanza yananunuliwa kwa fedha za kigeni na hivyo kuporomoka kwa Shilingi, kuliongeza gharama za ununuzi na pia bei yake kimataifa, ina tabia ya kubadilikabadilika, tofauti na gesi inayochimbwa nchini.

Capacity Charge Ngamlagosi alisema mbali na faida ya kutumia umeme unaotokana na gesi, ambao kwa mujibu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), karibu asilimia 70 ya umeme wote kwa sasa ni wa gesi, pia walibaini mitambo yote ya kufua umeme wa dharura imeondolewa.

“Ni kweli Tanesco hivi sasa wanatumia kiasi kidogo cha mafuta na mitambo yote ya dharura haitumiki tena, pia vyanzo vya nishati vimeongezeka na vingi ni vya uhakika na hakuna kampuni ya dharura ya muda mfupi inayolipwa tozo ya uwezo wa mtambo (capacity charge),” alisema Ngamlagosi.

Tozo hiyo ya uwezo wa mtambo, ambayo ilikuwa ikitozwa katika mitambo mingi ya ufuaji umeme wa dharura, iliongeza gharama kwa kuwa hata kama mtambo hauzalishi au umezimwa kabisa, tozo hiyo ilikuwa ikilipwa kwa siku kwa mabilioni ya Shilingi.



ZeroDegree.
TANESCO yasamehe jumla ya shilingi bilioni 69 kwa Watanzania. TANESCO yasamehe jumla ya shilingi bilioni 69 kwa Watanzania. Reviewed by Zero Degree on 4/03/2016 11:27:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.