Loading...

47% ya Walimu ni watoro madarasani [ Soma Utafiti wa REPOA hapa. ]


Dar es Salaam. Taasisi ya Utafiti ya Repoa, imesema asilimia 47 walimu ya shule za msingi nchini hutoroka kufundisha darasani, hivyo kutishia mustakabali wa ubora wa elimu. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa, Dk Donald Mmari alisema sababu zinazochagiza utoro huo huenda ni motisha kidogo wanaopata walimu, hivyo wanaamua kufanya shughuli nyingine ili kujiongezea kipato.

Hayo yalibainishwa katika utafiti wa Repoa uitwao ‘Tanzania; Viashiria vya utoaji huduma’ uliojikita kwenye maeneo matatu; kuangalia uwapo wa vitendea kazi, uwezo wa watoa huduma na juhudi zao za utoaji huduma kwa sekta ya elimu na afya.

“Lakini inawezekana ni udhaifu katika usimamizi wa shule na ukaguzi mdogo, wanaona hakuna wa kuwafuatilia, sasa imefika wakati wa kuongeza ukaguzi na motisha itakayopunguza ukali wa maisha,” alisema Dk Mmari.

Katika utafiti huo uliofanyika 2014 na kujikita kwenye sekta ya afya na elimu, ulihusisha sampuli ya shule 400 na zahanati 400 kwa mikoa yote nchini. Akiwasilisha ripoti hiyo jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi wa Utafiti wa Repoa, Dk Lucas Katera alisema walimu waliweza kujibu kwa usahihi asilimia 59 ya maswali ya masomo ya Kiingereza na hisabati.

Mkurugenzi wa Sekta ya Jamii, Ofisi ya Rais, Kitengo cha Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Linda Ezekiel alitaja maeneo matatu ya uhitaji yanayoweza kusaidia ufanikishaji changamoto kwa sekta hizo.

Linda alitaja mambo hayo ni kuhakikisha uwapo wa bajeti ya kutosha, kuongeza uwajibikaji na ukaguzi pia kutoa mikataba ya kuwabana watumishi kufikia malengo.




ZeroDegree.
47% ya Walimu ni watoro madarasani [ Soma Utafiti wa REPOA hapa. ] 47% ya Walimu ni watoro madarasani [ Soma Utafiti wa REPOA hapa. ] Reviewed by Zero Degree on 5/29/2016 10:54:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.