Loading...

Makamu wa rais awataka wafugaji waliovamia maeneo ya hifadhi kuanza kuondoka.


Baadhi ya wakuu wa mikoa waliopewa agizo la kusimamia zoezi la kuondoa mifugo zaidi ya milioni tano iliyoko kwenye maeneo ya hifadhi wamesema watahakikisha wanatumia sheria zilizopo kufanikishazoezi hilo na wameendelea kuwataka wale wote walioko kwenye maeneo hayo kutoka kwa hiyari yao ili kuepusha madhara na malalamiko yasiyo ya lazima.

Akizungumzia agizo hilo mkuu wa mkoa wa Simiyu ambao ni miongoni mwa inayoguswa na agizoa hilo Bw Antony Mtaka amesema pamoja na changamoto zilizopo ikiwemo ya kulazimika kutumia nguvu agizo hilo linatekelezeka kwani ni utekelezaji wa sharia halali ambazo zinapaswa kuheshimiwa na kima mmoja.

Agizo la kuondoa mifugo iliyoko ndani ya hifadhi ilitolewa na makamu wa rais Mh Samia Suluhu Hassan wakati anakabidhi hundi ya shilingi bilion moja iliyotolewa na shirika la hifadhi za taifa (TANAPA) kwa ajili ya kununulia madawati 16,000 katika wilaya 54 za mikoa 19 inayopakana na hifadhi ambaye pia aliagiza zoezi hilo liende sambamba na kutenga maeneo ya malisho kwa mifugo itakayoondolewa na ile ya nje ya nchi kurudi ilikotoka.

Mh makamu wa rais alisema wakati wafugaji wa hapa nchini wakihangaika na mifugo kutafuta malisho tafiti zinaonyesha kuwa mifugo zaidi ya milioni tano iliyotoka nchi jirani imeingia nchini kupitia mikoa ya Arusha, Geita, na Kagera, na inalishwa katika maeneo ya hifadhi utaratibu aliosema kuwa hauvumiliki.

Akizungumza katika haflka hiyo waziri wa maliasili asili Mh Prof Jumanne Maghembe amesema baada yakukabidhi mchango huo wa fedha za madawati yatakayowasaidia wanafunzi zaidi ya 49,000 hatua itakayofuata ni kukabidhi shehena ya magogo ya kutengenezea madawati hayo na kwamba wizara imejipanga kuhakikisha maliasili zinalindwa na zinatumika kwa manufaa ya wote.




ZeroDegree.
Makamu wa rais awataka wafugaji waliovamia maeneo ya hifadhi kuanza kuondoka. Makamu wa rais awataka wafugaji waliovamia maeneo ya hifadhi kuanza kuondoka. Reviewed by Zero Degree on 5/18/2016 10:01:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.