Makonda awatoa hofu walimu juu ya sakata la mabasi ya mwendo kasi, awataka kuwa na subira wakati utaratibu wakuwasaidia ukifuatiliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatoa hofu walimu wanaotumia mabasi ya mwendo kasi kuwa na subira ili waangalie utaratibu wa kuwasaidia walimu hao, ambao awali walikuwa wakipanda daladala bila kulipa nauli.
Amesema ni mapema kuanza kuzungumzia suala la walimu katika mabasi yaendayo kasi, hivyo amewataka walimu wanaotumia usafiri huo kuwa na subira kwa kipindi hiki.
“Mradi huu wa UDART ndio kwanza unaanza na bado una changamoto zake, hatuwezi kusema leo walimu waanze kupanda bure, mabasi haya pia yana uongozi wake na taratibu zake, lazima tukae tuzungumze nao ili tuone tutafanyaje kuhusu walimu,” alisema Makonda.
Aliongeza kuwa Serikali inamiliki kwa asilimia 49 katika UDART na wenye mradi huo wanamiliki asilimia 51, hivyo lazima kuwepo na utaratibu ambao pande zote kukubaliana kuhusu suala la walimu.
Kauli hii ya Makonda imekuja baada ya mradi huo wa mabasi yaendayo kasi, kutoitambua ofa ya walimu hao kupanda bure.
ZeroDegree.
Makonda awatoa hofu walimu juu ya sakata la mabasi ya mwendo kasi, awataka kuwa na subira wakati utaratibu wakuwasaidia ukifuatiliwa.
Reviewed by Zero Degree
on
5/20/2016 10:04:00 AM
Rating: