Loading...

MARUFUKU kwa Kampuni KUNUNUA SHAMBA na kupima Viwanja.


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amepiga marufuku ununuzi wa mashamba, unaofanywa na kampuni binafsi na kuyapima kuwa viwanja. 

Akihitimisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya wizara hiyo, Lukuvi alisema atakayenunua shamba, anapaswa kuhakikisha linabaki hivyo na kama anataka liwe viwanja, ni vema akakabidhi halmashauri libadilishwe matumizi.“Kama kuna mtu binafsi amenunua mashamba kwa lengo la kupima viwanja imekula kwako kabidhi halmashauri itapanga, kupima na kumilikisha wenyewe kwani kuna watu wanakuja na brief case zao na kutajirika kwa kupima viwanja,” alisema Lukuvi.

Lukuvi aliagiza halmashauri kutofikiri ardhi ni kwa ajili ya kujitajirisha pekee na kusisitiza kuwa kuanzia sasa hati za viwanja zitatolewa baada ya mwezi mmoja badala ya ilivyokuwa awali miaka miwili.

Akizungumzia ujenzi holela, alisema awali serikali ilikuwa na jukumu la kupima na upangaji pekee yake, lakini hawakufanya vya kutosha jambo lililosababisha wananchi kuwatangulia na kujenga.

Kuhusu utoaji hati, alisema ofisini kwake kuna hati zaidi ya 4, 800 za watu waliokuwa hawajachukua wakiwemo walio nje ya nchi. Alisema mlundikano huo wa hati, unatokana na hisia za wamiliki kudhani zingechukua muda mrefu.

Alisisitiza wahusika waende kuzichukua. na kuwataka kwenda kuchukua. Lukuvi alisema kuanzia sasa utoaji hati utaishia wilayani baada ya kugawa mamlaka kwenye kanda kanda nane ambako yuko msajili atakayesaini.




ZeroDegree.
MARUFUKU kwa Kampuni KUNUNUA SHAMBA na kupima Viwanja. MARUFUKU kwa Kampuni KUNUNUA SHAMBA na kupima Viwanja. Reviewed by Zero Degree on 5/25/2016 12:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.