Loading...

Mawaziri wacharuka kuhusu suala la Jeshi kuhusishwa na Siasa.


MAWAZIRI wa Serikali ya Awamu ya Tano wamewajia juu wabunge wa upinzani na wananchi wanaovishutumu kila mara vyombo vya ulinzi nchini na kuwataka kuacha kuvihusisha vyombo hivyo na masuala ya kisiasa.

Mawaziri hao ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.

Wamewataka wananchi na hususani wabunge wa vyama vya upinzani, kutambua kuwa vyombo hivyo vya ulinzi ambavyo ni pamoja na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi wajibu wake mkubwa ni kulinda mipaka ya nchi na usalama wa raia na mali zao.

Akizungumza wakati wa mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara inayoshughulikia Muungano na Mazingira, Dk Mwinyi alisema haijawahi kutokea na wala haitotokea jeshi kutumika kisiasa.

Alisema Jeshi la Tanzania limekuwa likitekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria iliyojiwekea pamoja na za kimataifa na wala hata siku moja haliwezi kutumika kwa ajili ya kutumiza malengo ya kundi fulani.

“Jeshi letu lina sifa ya kimataifa ya ulinzi wa amani, dunia kote tunasifika kwa weledi, kulinda amani na mipaka yetu. Haijawahi kutokea wala haitotokea jeshi kujiingiza kwenye shughuli za kisiasa,” alisisitiza Dk Mwinyi.




ZeroDegree.
Mawaziri wacharuka kuhusu suala la Jeshi kuhusishwa na Siasa. Mawaziri wacharuka kuhusu suala la Jeshi kuhusishwa na Siasa. Reviewed by Zero Degree on 5/04/2016 01:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.