Loading...

Polisi wawili matatani kwa kuomba na kupokea RUSHWA ya zaidi ya milioni 7.


POLISI mkoani Rukwa inawashikilia askari wake wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi wilayani Nkasi, wakituhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh milioni 7.2 wamsaidie mtuhumiwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Rukwa, Leonce Rwegasira alitaja askari hao kuwa ni Konstebo Filbert Ruhemeja na Konstebo Bahati Sengerema, ambao walikuwa wakifanya kazi katika Kituo cha Polisi mjini Namanyere wilayani Nkasi.

Alisema polisi inawafanyia uchunguzi wa kina askari wake wawili, wanaotuhumiwa kwa kashfa ya kuomba rushwa ya Sh milioni 7.2 na iwapo watabainika halitasita kuwatimua na kuwafikisha mahakamani.

.Alisema askari hao wawili wa polisi, wanatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya fedha kutoka kwa mtu mmoja (jina linahifadhiwa) ili wamsaidie katika shitaka linalomkabili.

Source: Mtembezi




ZeroDegree.
Polisi wawili matatani kwa kuomba na kupokea RUSHWA ya zaidi ya milioni 7. Polisi wawili matatani kwa kuomba na kupokea RUSHWA ya zaidi ya milioni 7. Reviewed by Zero Degree on 5/04/2016 12:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.