Loading...

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella awapa siku 7 wavuvi wilayani Sengerema kurejea kazini mara moja.


Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza, ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo John Mongella, imetoa siku saba kwa zaidi ya wavuvi 1,000 wa kisiwa cha Kasarazi Wilayani Sengerema wanaoendelea na mgomo wa shughuli za uvuvi katika Ziwa Victoria kurejea kazini mara moja. 



Huku ikiwaonya vikali baadhi ya wavuvi wanaodaiwa kupanga njama za kuwatosa majini wamiliki wa mitumbwi kutojaribu kufanya hivyo.

Mgogoro huo ulioanza kurindima Mei 26 mwaka huu, hatimaye umetua mikononi mwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye ameongozana na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama hadi katika Kijiji cha Kalebezyo, Halmashauri ya Buchosa kwa lengo la kusikiliza pande hizo mbili zinazohasimiana, ambapo kila upande umeeleza malalamiko yake.


Mongella akatoa msimamo wa serikali kuhusu kauli za vitisho zinazodaiwa kutolewa na baadhi ya wavuvi wa kisiwa hicho cha Kasarazi.

Mgogoro huo ulianza kufukuta Aprili mwaka huu, baada ya wamiliki wa vyombo vya uvuvi wapatao 150, waliowekeza katika Kisiwa cha Kasarazi kugundua kuwa wamekuwa wakipata hasara ya mamilioni ya shilingi kutokana na hujuma ya mapato ya uvuvi wa dagaa pamoja na mafuta inayodaiwa kufanywa na baadhi ya wavuvi wasio waaminifu.




ZeroDegree.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella awapa siku 7 wavuvi wilayani Sengerema kurejea kazini mara moja. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella awapa siku 7 wavuvi wilayani Sengerema kurejea kazini mara moja. Reviewed by Zero Degree on 5/29/2016 11:29:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.