Sukari yazidi kuwa adimu nchini, kila siku afadhali ya jana.
Mei 10 mwaka huu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema kiasi hicho cha sukari kimeingizwa na kuanza kusambazwa nchini. Alisema shehena nyingine ya tani 24,000 ingewasili nchini Mei 13 na tani nyingine 20,000 zingewasili baadaye.
Majaliwa alisema katika sukari hiyo, tani 2,000 zingepelekwa mikoa ya Kaskazini, tani 3,000 mikoa ya Kanda ya Ziwa, tani 2,000 mikoa ya Kusini, tani 2,000 mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na tani 2,000 mikoa ya Kanda ya Kati, lakini kote huko bado kuna upungufu wa bidhaa hiyo.
Upungufu huo katika maeneo mengi unatokana na wafanyabiashara kuigomea bei elekezi na kuacha kuagiza sukari kutoka nje ya mkoa, hivyo kuadimika kwa bidhaa hiyo.
Geita
Maeneo mengi ya wilaya za mkoa huo; Chato, Nyangwale na Geita hakuna sukari kabisa.
Kutokana na tatizo hilo, uongozi wa mkoa umelazimika kuiagiza katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera ambako wameahidiwa tani 90 zitakazosambazwa na kuuzwa kwa Sh2,200 kwa kilo tofauti na bei elekezi ya Sh1,800.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie alisema mkoa umechukua hatua hiyo kutokana na sukari iliyoingizwa nchini kutoka nje kuwa na gharama kubwa.

“Taarifa tulizozipata kutoka kwa msemaji wa kampuni ya Tanzania Commodities Trading Co.Ltd inaeleza mfuko wa kilo 25 utauzwa kwa Sh45,000 na wafanyabiashara wataichukulia Dar es Salam, ukipiga hesabu wao watalazimika kununua kwa bei ya jumla ya Sh1,800 sasa wakiisafirisha hadi huku lazima bei itakuwa kubwa zaidi,” alisema.
Mangochie aliyezungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga alisema tayari wametoa maagizo kwa wafanyabiashara watakaonunua sukari kwa mawakala kuorodhesha majina ya wafanyabiashara wadogo watakaonunua bidhaa hiyo na kiasi wanachochukua ili maofisa biashara wa halmashauri waweze kufuatilia bei.
Mkazi wa Geita, Pascazia Mongi alisema kutokana bidhaa hiyo kutokuwapo madukani bei ya kikombe cha chai kwenye migahawa imepanda kutoka Sh200 hadi Sh500.
Arusha
Mkoani Arusha, baadhi ya wakazi wamelazimika kwenda katika duka la Chuo cha Jeshi wilayani Monduli kusaka bidhaa hiyo.
Uchunguzi uliofanywa katika maduka makubwa kama Nakumatt, Sakina na Arusha Modern na mengine ya kawaida umebaini sukari imekuwa adimu na kusababisha wanaojishughulisha na biashara ya chai kusitisha huduma hiyo.“Nina siku tatu nyumbani kwangu watoto wanakwenda shule bila kunywa chai, nimelazimika kwenda Monduli kutafuta sukari,” alisema Baraka Shija, mkazi wa Mbauda.
Mkazi wa Monduli, Lilian Mollel alisema imebidi kutembea umbali mrefu kutoka Monduli kwenda mjini Arusha kusaka sukari. “Nimezunguka siku nzima sijapata, mimi niko tayari kununua kwa bei yeyote,” alisema.
Diwani wa Kimaonduli, Ruben Ngowi alisema upatikanaji wa sukari katika kata hiyo si wa kuridhisha.
Mara
Wafanyabiashara mkoani Mara walisema licha ya Serikali kutoa agizo la kuwaruhusu kusambaza sukari, bado hawajapewa vibali kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye alisema wafanyabiashara hawajapewa vibali na hawajapokea sukari iliyosambazwa na Serikali.
Alisema hata juzi alipiga simu kuulizia kama sukari imeanza kusambazwa, lakini alijibiwa kuwa bado kutokana na vibali kuchelewa.
Alisema kuna mfanyabiashara mmoja ambaye ameagiza tani 25 ambazo ziko njiani, lakini hofu yake ni kwamba huenda bei itakuwa juu kuliko iliyopangwa na Serikali.
Kilimanjaro
Wakazi wa mji wa Moshi wameitaka Serikali kuweka maduka maalumu ya kuuzia bidhaa hiyo badala ya kusambaza kwa mawakala ambao si waaminifu.
Mmoja wa wakazi hao, Amos Shao alisema: “Kwa sababu Serikali imeamua kuchukua jukumu la kusambaza sukari, waweke katika maduka yao ambayo wananchi tutakwenda kuinunua kwa sababu wanaposambaza kwa mawakala sisi haitufikii,” alisema.
Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema jana kuwa ndani ya wiki hii, tani 15,000 za sukari zitaingia sokoni kukabiliana na uhaba uliopo.
Sumbawanga
Wakizungumza jana, baadhi ya wakazi wa Sumbawanga mkoani Rukwa walisema licha ya uhaba, bei ya sukari imepanda katika maduka ya rejareja kutoka Sh2,200 kwa kilo hadi 3,800.
Mkazi wa Majengo, Sarafina Juma alisema kupaa kwa bei ya sukari kumewafanya waache kunywa chai kwa kuwa wanashindwa kumudu kununua.

Manyara
Kutokana na uhaba wa sukari, baadhi ya wakazi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Manyara wanatumia asali au sukari guru katika chai.
Mkazi wa Dagailoi, Eva Anthony alisema alinunua sukari kilo kwa Sh4,000 wiki mbili zilizopita na sasa amezunguka madukani na kuikosa hivyo ameamua kutumia sukari guru.
Mkazi wa Nyunguu, Hamis Hussein alisema kilo moja inauzwa kwa Sh5,000 au Sh4,500 tofauti na Sh2,000 za awali.
Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Sukari yazidi kuwa adimu nchini, kila siku afadhali ya jana.
Reviewed by Zero Degree
on
5/19/2016 11:28:00 AM
Rating: