Loading...

Ted Cruz ajitoa kwenye kinyang'anyiro cha uteuzi kugombea nafasi ya urais Marekani.



Cruz ameshindwa kwenye mchujo Indiana.

Seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz amejiondoa katika kinyang'anyiro cha uteuzi kugombea nafasi ya urais wa Marekani kupitia chama cha Republican.



Alitoa tangazo lake punde tu baada ya kupoteza kura katika kampeni za mwisho Indiana.

Cruz amewaambia wafuasi wake kuwa alifanya kila analoweza katika kampeni 

zake,lakini hakukuwa na njia ya yeye kuweza kusonga mbele zaidi.

Mwandishi wa BBC aliyepo katika vituo vya kupigia kura Indiana amesema wafuasi wa Cruz wamestushwa na kukatishwa tamaa.


Trump ana nafasi nzuri ya kushinda uteuzi.

Tangazo hilo linatoa mwanya kwa Donald Trump kupata uteuzi wa chama chake cha Republican.

Source: BBC





ZeroDegree.
Ted Cruz ajitoa kwenye kinyang'anyiro cha uteuzi kugombea nafasi ya urais Marekani. Ted Cruz ajitoa kwenye kinyang'anyiro cha uteuzi kugombea nafasi ya urais Marekani. Reviewed by Zero Degree on 5/04/2016 12:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.