Loading...

Utaratibu na Tarehe kamili ya kuchukua fomu YANGA huu hapa.


Baada ya TFF kutangaza rasmi uchaguzi wa klabu ya Yanga kufanyika June 25 mwaka huu, timu hiyo imetangaza tarehe ambayo fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi zitaanza kutolewa.

Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit ameweka wazi tarehe ya kuchukua fomu ni Mei 27 wakati tarehe ya kurejesha ni Mei 29.

Baraka amesema baada ya zoezi hilo Kamati ya uchaguzi itaanza kusikiliza pingamizi zitakazokuwa zimewasilishwa huku orodha ya mwisho ya wagombea waliopitishwa ikitarajiwa kutangazwa Juni Mosi.

“Tunataka kwenda na muda ambao tumepangiwa na BMT na TFF, ndiyo maana mchakato huu tunauweka wazi kwa ajili ya Wanachama wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali waweze kuingia kwenye kuchukua fomu za kugombea,” amesema Baraka.




ZeroDegree.
Utaratibu na Tarehe kamili ya kuchukua fomu YANGA huu hapa. Utaratibu na Tarehe kamili ya kuchukua fomu YANGA huu hapa. Reviewed by Zero Degree on 5/05/2016 09:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.