Loading...

Watanzania WASHAURIWA kuwa na subira juu ya suala la BUNGE kurushwa live.


Katibu Mkuu wa National Reconstruction Alliance (NRA), Hassan Kisabya Almas amewataka Watanzania wanaoomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonyeshwa kupitia matangazo ya moja kwa moja (Live) kuomba kwa utaratibu bila kuharibu amani ya Tanzania kwani ni hazina pekee iliyopo ambapo nchi nyingine zinatamani kuwa nayo.

Almas aliyasema hayo jana alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO).

“Leo hii tupo tunaopigania kutaka kuona Bunge Live, lakini yote haya ni kwa kuwa Tanzania amani tunayo, sidhani nchi kama Afghastan kuna siku watakayoamua kuonyesha Bunge Live kwa mwaka mzima kwa saa 24, kama wataweza kukaa kuangalia Bunge hilo, hivyo basi wale wanaotaka hayo, kwanza tudumishe amani yetu,” alisema Almas.

Almas alieleza kuwa yeye ni muumini wa wanaotaka kuona Bunge likioneshwa ‘live’ lakini hashadadii kama inavyofanywa na watu wengine kwa sababu amani ya Tanzania ni zaidi ya dhahabu ambayo Tanzania inajivunia hivyo ni lazima Watanzania kuitunza na kuithamini amani ambayo ipo kwa sasa na kuacha kuchochea mambo ambayo yanaweza kuleta machafuko katika nchi na amani ambayo leo haithaminiwi ikaja kukumbukwa siku moja.

Vilevile, amewataka Waandishi wa Habari kuandika yale yaliyo mazuri ya nchi kuliko mabaya machache ili kuzidi kuitangaza Tanzania vyema kimataifa, kwani sio uzalendo kuona mambo yote mabaya yanakuwa kurasa za mbele za magazeti, bali kwanza yarekebishwe kwa kuwa ni makosa yanayoweza kurekebishwa. Kalamu za Waandishi wa Habari ni chachu ya amani na maendeleo ya Taifa la Tanzania.




ZeroDegree.
Watanzania WASHAURIWA kuwa na subira juu ya suala la BUNGE kurushwa live. Watanzania WASHAURIWA kuwa na subira juu ya suala la BUNGE kurushwa live. Reviewed by Zero Degree on 5/05/2016 10:24:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.