Loading...

AJALI: Basi moja la mwendokasi lagonga mlemavu wa viungo na kumsababishia kifo papo hapo.


Dar es Salaam. Mlemavu wa viungo amegongwa na basi la mwendokasi na kufa papo hapo jana usiku, eneo la Kariakoo.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Lucas Mkondya amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 2.00 usiku makutano ya barabara za Msimbazi na Uhuru na kwamba, mwili wa mlemavu huyo wa kiume umeokotwa vipandevipande. 

Nkondya amesema chanzo cha ajali ni mwendokasi wa dereva, kwani tukio hilo limetokea karibu na makutano ya barabara za Msimbazi na Uhuru ambako kuna mataa, hivyo alitegemea basi lingekuwa kwenye mwendo wa kawaida.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
AJALI: Basi moja la mwendokasi lagonga mlemavu wa viungo na kumsababishia kifo papo hapo. AJALI: Basi moja la mwendokasi lagonga mlemavu wa viungo na kumsababishia kifo papo hapo. Reviewed by Zero Degree on 6/11/2016 10:36:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.