Barabara 12 KUJENGWA Kiwalani na Benki ya Dunia.
BARABARA za mitaa ya kata ya Kiwalani, zinatarajiwa kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami baada ya Benki ya Dunia kutoa fedha kwa ajili ya mradi huo. Awali mradi wa ujenzi wa barabara 12 za mitaa ya kata hiyo, ulikwama kutokana na kuwepo kwa nyumba hewa 45 ambazo ziliingizwa kulipwa fidia kwa ajili ya kupisha ujenzi wa barabara hizo.
Akizungumza na wananchi wa kata yake katika mkutano wa kuwashukuru kumchagua kuwa diwani wa kata hiyo, Mussa Kafana alisema, tayari jambo hilo limeshawekwa sawa.
Alisema tayari wananchi ambao nyumba zao zilipaswa kupisha ujenzi wa barabara hizo, wameanza kulipwa fidia. “Tayari fedha zimeshatolewa na kusainiwa na Meya (Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko) na huo mradi utajengwa katika awamu mbili, ya kwanza itahusisha barabara sita na awamu ya pili zitajengwa nyingine sita,” alisema Kafana.
Katika hatua nyingine, Kafana alisema amepata Sh milioni 90 kufanya ukarabati wa shule ya sekondari Bwawani, ambayo tangu ijengwe mwaka 2000 haikuwahi kutumiwa kutokana na kujaa maji.
ZeroDegree.
Barabara 12 KUJENGWA Kiwalani na Benki ya Dunia.
Reviewed by Zero Degree
on
6/01/2016 10:20:00 AM
Rating: