Bodaboda zachangia Kuongezeka kwa MSONGAMANO Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kuongezeka kwa ajali za pikipiki nchini kumesababisha msongamano mkubwa katika hospitali ya muhimbili na kusababisha huduma kuzorota kutokana na changamoto hiyo ingawa taasisi hiyo imekuwa ikijitahidi kutoa matibabu ikiwa na kuwaongezea ujuzi zaidi madaktari wanaohudumu katika hospitali hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwake hospitalini hapo mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo,DR.OTHMAN KILOLOMA,amesema hali hiyo inatokana na ongezeko la vyombo vya usafiri kama bodaboda na ongezeko la magari ya watu binafsi ambalo ndilo linachangia kutokea kwa ajali nyingi.
Amesema taasisi hiyo kwa kushirikiana na taasisi ya GLOBAL ORTHOPAEDICS AND TRAUMATOLOGY ya nchini MAREKANI inatoa mafunzo kwa madkatari wa hapa nchini katika njia mpya za kukabiliana na utabibu wa magonjwa ya mifupa inayotokana na ajali na madaktari wanaotoka nje ya nchi ambao wameletwa na nchi zao baada ya sifa nzuri ya taasisi kusikika.
Kwa upande wake DK KENNEDY NCHIMBI kutoka taasisi hiyo aliewaongoza waandishi wa habari kushuhudia mafunzo yanavyotolewa kwa madaktari hao kutoka nchi za Africa namna ambavyo upasuaji mbalimbali unavyofanywa kurekebisha halizao,amesema mafunzo hayo yana lengo la kukabiliana na hali hiyo ya ongezeko la ajali lakini ni kuwatayarisha madaktari wanaotoka mikoani kukabiliana na hali hiyo maneo yao kabla ya kuja MOI.
ZeroDegree.
Bodaboda zachangia Kuongezeka kwa MSONGAMANO Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Reviewed by Zero Degree
on
6/04/2016 10:51:00 AM
Rating: