Chuo Kikuu cha Dar es Salaam [ UDSM ] kutumia Kiswahili kama lugha rasmi ya mawasiliano.
Dar es Salaam. Februari 3, 2009, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete alihutubia mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Ethiopia alipokuwa akihitimisha uenyekiti wake na kumkabidhi kiongozi wa zamani wa Libya, Muamar Gadaffi.
Juni 16, mwaka huu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa bungeni alisema Serikali inatarajia kuanza kutumia Kiswahili katika mikutano yote ya kimataifa itakayowakilishwa na viongozi wake baada ya kutuma wataalamu watakaokitafsiri kwa watumiaji wa lugha nyingine duniani.
Katika kuunga mkono juhudi hizo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimetangaza kutumia Kiswahili kama lugha rasmi ya mawasiliano chuoni hapo ikiwa ni kuunga mkono kauli hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), Tawi la UDSM, Salifius Mligo jana alimpongeza Majaliwa kwa matumizi na kukuza matumizi ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.
Alisema katika kutekeleza agizo hilo, UDSM kupitia baraza lake lililokutana Machi 30, mwaka jana lilipitisha makubalino ya kutumia lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya mawasiliano chuoni hapo.
Akizungumzia faida ya kujifunza lugha ya Kiswahili kama taaluma, Profesa Aldin Mutembei alisema inaongeza wigo wa ajira kutokana na kupanuka kwa matumizi ya yake katika nchi nyingi.
Alisema uamuzi wa kutumia lugha hiyo katika mikutano ya ndani na nje ya nchi utalitangaza Taifa.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam [ UDSM ] kutumia Kiswahili kama lugha rasmi ya mawasiliano.
Reviewed by Zero Degree
on
6/25/2016 12:46:00 PM
Rating: