Loading...

CUF: POLISI inachanganya majukumu yake na Siasa.


Makamu wa kwanza wa rais mstaafu wa Zanzibar ambaye pia ni katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharrif Hamad amehojiwa na jeshi la polisi Zanzibar katika jengo la makao makuu ya jeshi hilo yaliyoko ziwani chini ya ulinzi mkali wa polisi.



Maalim Seif ambaye aliitikia wito wa jeshi hilo la kutakiwa kufika makao makuu alifika wakati wa saa tatu na nusu asubui na huku jengo hilo likiwa barabara zake zote zimefungwa na polisi kutoruhusu mtu yeyote kuingia maeneo hayo na alitoka ndani ya jengo hilo mnao saa sita akiwa na msafara wa magari matatu.

Naibu mkurugenzi wa upelelezi na makosa ya jinai Zanzibar kamishna msaidizi Salum Msangi akiongea na vyombo vya habari baada ya mahojiano hayo amesema kiongozi huyo mstaafu ametoa ushirikiano mzuri na polisi kwa sasa inaangalia na kupitia mahojiano hayo na baadaye watatoa tamko rasmi la hatua zipi zitakazofuata ingawa amesema sababu kubwa ya mahojiano hayo ni kutokana na kauli za mwanasiasa huyo za hivi karibuni ingawa hakuzitaja.

Hata hivyo kwa upande wao chama cha wananchi CUF kimelani kitendo hicho ambacho wamesema ni kinyume na maadili ya uongozi ambapo mkuruegnzi wa uenezi na mahusiano ya umma Salum Bimani amesema polisi wameanza kuacha majukumu yao na kujiingiza katika siasa na kutekeleza shinikizo la watawala.

Mji wa Zanzibar umeendelea kuwa shwari pamoja na baadhi ya maduka wakati wa asubui kufungwa lakini hali baadaye ilirejea kama kawaida huku kiongozi huyo wa CUF akiendelea na ziara yake ya kichama katika mikoa mitatu ya Unguja.

Source: Mtembezi





ZeroDegree.
CUF: POLISI inachanganya majukumu yake na Siasa. CUF: POLISI inachanganya majukumu yake na Siasa. Reviewed by Zero Degree on 6/01/2016 10:54:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.