Loading...

Giggs aamua kuondoka Man U.


Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United, Ryan Giggs.

Baada ya miaka 29 ya kuichezea Manchester United, mchezaji wa zamani wa klabu hiyo ambaye amekuwa kocha msaidizi kwa makocha wawili waliopita katika timu hiyo, David Moyes na Loius Van Gaal, mkongwe wa Manchester United, Ryan Giggs amefanya uamuzi wa kuondoka katika klabu hiyo.

Giggs amekataa kuendelea kufanya kazi na Man United sababu kubwa ikielezwa kuwa uongozi wa Man United ulimuahidi kuwa baada ya kuondoka Moyes na Van Gaal angepatiwa nafasi ya juu katika klabu hiyo lakini hali imekuwa tofauti na nafasi hiyo kupewa Jose Mourinho.

Inasemekana kwasasa wawakilishi wa Giggs kwa sasa wanafanya mazungumzo wa Man United ili kumwachia huru Giggs ili akafanye kazi sehemu nyingine ambayo atapatiwa nafasi ambayo anahitaji.

Baada ya kuachana na Man United, Alhamisi ya Juni, 30 Giggs anataraji kuanza kufanya vipindi vya uchambuzi wa soka kuhusu mashindano ya Uefa Euro yanayoendelea nchini Ufaransa katika moja ya kituo cha tv huku akisubri kibarua kipya atakachokipata.

Pamoja na kuondoka, Giggs ataendelea kuwa mchezaji ambaye amecheza michezo mingi katika klabu ya Man United kwa kucheza michezo 963 na kushinda vikombe 19.


ZeroDegree.
Giggs aamua kuondoka Man U. Giggs aamua kuondoka Man U. Reviewed by Zero Degree on 6/30/2016 09:46:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.