Loading...

Hatima ya kesi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo [ CHADEMA ] dhidi ya polisi kujulikana leo.


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Mwanza. Hatima ya kesi iliyofunguliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) dhidi ya polisi kupinga amri ya kupiga marufuku kufanyika maandamano na mikutano ya kisiasa nchini itajukana leo, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza itakapotoa uamuzi wa pingamizi la awali lililowekwa upande wa Serikali.

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Jaji Mohamed Gwae anayesikiliza shauri hilo baada ya upande wa utetezi unaowakilishwa na mawakili Robert Kidando na Obadia Kajungu kuweka pingamizi ukiomba Mahakama itupilie mbali kesi hiyo kwa madai ina mapungufu kisheria. 

Katika hoja zao mawakili hao wanaowawakilisha wadai wawili, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanadai mleta maombi (Chadema) kupitia kwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho hawakunukuu kifungu cha 5(1)(2) ambacho kingeipa Mahakama mamlaka ya kusikiliza na kutoa uamuzi kuhusiana na ombi hilo.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Hatima ya kesi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo [ CHADEMA ] dhidi ya polisi kujulikana leo. Hatima ya kesi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo [ CHADEMA ] dhidi ya polisi kujulikana leo. Reviewed by Zero Degree on 6/21/2016 10:22:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.