Loading...

Mgombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump anusurika kuuawa.


Mwanamume mmoja raia wa Uingereza anayetuhumiwa kwa kupora bunduki ya afisa mmoja wa polisi katika mkutano wa kisiasa wa Donald Trump, amewaambia wapelelezi wa Marekani kuwa, alitaka kumpiga risasi na kumuuwa mgombea huyo wa kiti cha Urais wa chama cha Republican.

Kwa mjibu wa stakabadhi za mahakama, Michael Sandford anasema kuwa aliendesha gari hadi Las Vegas akiwa na nia ya kumpiga risasi Bw Trump siku ya Jumamosi. Awali Donald Trump alimtimua Meneja wake wa kampeni Corey Lewandowski kwa kutofautiana naye katika kauli zake.


Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden amemlaum Trump kwamba kauli zake ni za hatari.

Source: BBC Swahili
ZeroDegree.
Mgombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump anusurika kuuawa. Mgombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump anusurika kuuawa. Reviewed by Zero Degree on 6/21/2016 10:16:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.