Hatimaye BAJETI ya Trilioni 29.5 yapitishwa bila UPINZANI Bungeni.
Bunge limepiga kura na kupitisha bajeti ya serikali yenye jumla ya shilingi Trilioni 29.5 kwa mwaka wa fedha 2016/17 licha ya wabunge wa kambi ya upinzani kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakiwa wamebandika karatasi kuziba midomo yao.
Kwa takribani siku 23, tangu May 30 mwaka huu wabunge wa kambi ya upinzani wamesusia kushiriki katika vikao vya bunge ambapo Juni 20 ikiwa ni siku ya kuhitimisha mjadala wa bajeti wabunge hao wameamua kuziba midomo kwa gundi na karatasi na kutoka nje ya ukumbi wakilalamikia uendeshaji na bunge hilo.
Akijibu hoja ya bunge kuwa Raba Stempu, mwanasheria mkuu wa serikali George Maseju amepinga hoja ya bunge kuwa Raba Stempu amesema chombo kinachoendeshwa kwa majadiliano kinahitaji umhimu wa kuzingatia katiba na sheria na kwa kuwa ni kiunganishi cha wananchi na serikali yao.
Waziri wa fedha na uchumi, Mhe. Dkt Phillip Mpango.
Akijibu hoja za wabunge waziri wa fedha na uchumi Mhe Dkt Phillip Mpango amesema serikali haitaongeza tozo katika mafuta na itajielekeza katika kuimarisha miundombinu ya miradi, aidha amesisitiza serikali imeondoa msamaha wa kodi kwa mafao ya viongozi wa kisiasa na kusisitiza kuanzia sasa kiinua mgongo cha wabunge, mawaziri, rais, wakuu wa mikoa na wilaya vitatozwa kodi ili kujenga misingi ya usawa na haki.
ZeroDegree.
Hatimaye BAJETI ya Trilioni 29.5 yapitishwa bila UPINZANI Bungeni.
Reviewed by Zero Degree
on
6/21/2016 10:02:00 AM
Rating: