Loading...

JK kung'atuka MADARAKANI rasmi ifikapo tar 23 Julai mwaka huu.


HATIMAYE kitendawili cha lini makabidhiano ya kijiti cha Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yatafanyika, kimeteguliwa baada ya chama hicho tawala nchini kutangaza tarehe rasmi ya Mkutano Mkuu Maalumu wa kukabidhiana hayo.

Hatua ya kutangazwa kwa tarehe rasmi ya mkutano huo imekuja bada ya Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi jana katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya Chama, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete.


Christopher ole Sendeka

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi hizo, Msemaji wa chama hicho, Christopher ole Sendeka alisema Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho unatarajiwa kufanyika Julai 23, mwaka huu.

Alisema uamuzi wa kufanyika kwa mkutano huo imefikiwa baada ya kikao cha Kamati Kuu kuridhishwa na maandalizi yanayoendelea mjini Dodoma.

“Lengo kuu la Mkutano Mkuu huo Maalumu ni kukabidhiana kijiti cha uongozi wa juu wa chama chetu kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kwenda kwa Rais wa sasa Dk John Magufuli kama ulivyo utamaduni wa CCM,” alisema Sendeka.

Alisema mkutano huo ambao utajumuisha wajumbe 2,l430 kutoka nchi nzima utatanguliwa na vikao vya Sekretarieti, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa na kwamba mkutano huo utakuwa ni wa siku moja.

Aidha, alisema mkutano huo utahudhuriwa na wageni kutoka nje ya nchi, mabalozi, waasisi wa chama hicho, viongozi wakuu waastafu pamoja na vyama vyote vyenye usajili wa kudumu nchini.

“Mkutano huu unatarajiwa kuendeleza utamaduni wa CCM wa kukabidhiana kijiti cha uenyekiti kutoka kwa Kikwete kwenda kwa Rais Magufuli kama ilivyokuwa huko nyuma,” alisema.

Sendeka alifafanua kuwa kwa matakwa ya Katiba ya chama hicho, Rais Magufuli anatakiwa kupata nusu ya kura zote.

Source: Mtembezi
ZeroDegree.
JK kung'atuka MADARAKANI rasmi ifikapo tar 23 Julai mwaka huu. JK kung'atuka MADARAKANI rasmi ifikapo tar 23 Julai mwaka huu. Reviewed by Zero Degree on 6/19/2016 11:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.