Loading...

Polisi wazuia mahafali ya shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu Chadema [Tazama Video hapa ].


Naibu Katibu Mkuu wa Chadema , Salum Mwalimu.

Polisi mkoani Dodoma, wamezuia kufanyika kwa mahafali ya wanafunzi wanaounda Shirikisho la wanafunzi wa Vyuo Vikuu ambao ni wanachama wa Chadema yaliyopangwa kufanyika kwenye Hoteli ya African Dream.



Naibu Katibu Mkuu wa Chadema , Salum Mwalimu amesema wanafunzi saba wamekamatwa katika tukio hilo akiwamo Makamu wa Rais wa Udom, Rose Maluchu.


Polisi wamesema zuio hilo linatokana na kuzuka kwa ugonjwa wa ajabu katika Wilaya za Chemba na Kondoa ambako watu sita wanadaiwa kufariki dunia.

Mgeni rasmi katika Mahafali hayo alikuwa Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Frederick Sumaye.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Polisi wazuia mahafali ya shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu Chadema [Tazama Video hapa ]. Polisi wazuia mahafali ya shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu Chadema [Tazama Video hapa ]. Reviewed by Zero Degree on 6/19/2016 12:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.