Kila muamala wa fedha kulipa kodi serikalini, Rais Magufuli asisitiza.
RAIS John Magufuli ameziagiza taasisi zinazosimamia fedha na kodi, kuhakikisha kuwa serikali inakusanya kodi kwenye miamala ya fedha, inayofanywa na taasisi hizo na kampuni za simu na za madini.
Aidha, ameagiza kuwa Sh bilioni saba zilizolipwa kwa pensheni hewa, zirejeshwe mara moja huku akitoa ufafanuzi wa hatua ya serikali ya kusitisha kwa muda ajira serikalini.Rais Magufuli alisema hayo Dar es Salaam jana katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba na uzinduzi wa sarafu maalumu yenye thamani ya Sh 50,000 na vitabu viwili, kikiwemo vinavyozungumzia masuala ya fedha na uchumi.
Uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa BoT jijini Dar es Salaam, ulikwenda pamoja na kongamano lililojadili mada kuhusu namna ya kupata fedha za miradi ya maendeleo zaidi ya misaada na mikopo nafuu na athari zake iliyowasilishwa na Profesa Justin Lin wa Chuo Kikuu cha Peiking, China.
Rais Magufuli alisema takwimu zinaonesha katika mwezi mmoja wa Machi, miamala iliyofanywa na kampuni za simu za mkononi ni ya zaidi ya Sh trilioni 5.5, lakini alihoji ni kasi gani cha kodi kimeingia serikalini.
ZeroDegree.
Kila muamala wa fedha kulipa kodi serikalini, Rais Magufuli asisitiza.
Reviewed by Zero Degree
on
6/23/2016 12:41:00 PM
Rating: