Loading...

Kitengo cha watoto Hospitali ya Taifa ya Muhimbili [ MNH ] taabani.


Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa watoto wanaougua ugonjwa wa saratani waliolazwa katika jengo la watoto lililopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).



Dar es Salaam. Kitengo cha Watoto kilichopo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kinakabiliwa na upungufu wa vifaa tiba, hivyo kusababisha utendaji kuzorota na madaktari kutumia muda mrefu kuhudumia wagonjwa wachache.


Watoto 300 hulazwa kwenye kitengo hicho na uhudumia wengine 500 kliniki kwa siku, kinakabiliwa na upungufu wa mashine za kusaidia watoto kupumua, kupima mapigo ya moyo, joto na uzito.



Mkuu wa Idara ya Watoto, Dk Mary Charles.

Akizungumza jana wakati wa kupokea msaada wa vifaatiba kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) vyenye thamani ya Sh23 milioni, Mkuu wa Idara ya Watoto, Dk Mary Charles alisema changamoto kubwa kwa sasa inayowakabili vifaatiba ikilinganishwa na idadi ya watoto wanaopata huduma kwa siku.

Mkurugenzi Mtendaji wa GGM, Terry Mulpeter alisema lengo la kutoa msaada huo ni sehemu ya utaratibu wao kwa jamii inayowazunguka nchini.


Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Kitengo cha watoto Hospitali ya Taifa ya Muhimbili [ MNH ] taabani. Kitengo cha watoto Hospitali ya Taifa ya Muhimbili [ MNH ] taabani. Reviewed by Zero Degree on 6/29/2016 02:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.