Loading...

Mbunge aunga mkono hatua ya serikali kuongeza kodi kwa wanaoandika majina yao kwenye magari, ataka kodi iwe milioni 20.


Mbunge wa Korogwe Vijijini Steven Hillary Ngonyani ‘Maji Marefu’ amesema anaunga mkono hatua ya serikali kuongeza kodi kwa watu wote wanaoweka majina yao kama ‘Plate Number’ ili fedha hizo zisaidie wananchi wengine.

Ngonyani ameyasema hayo baada ya hotuba ya Waziri wa fedha Philip Mpango kuonyesha kwamba kwa watu wanaotaka majina yao yawe Plate Number watalipia milioni 10 kama kodi kutoka milioni 5 za awali.

”Mimi naona ni kitu cha kawaida kwa kuwa haiingiliani na namba za serikali hivyo hata wangeweka milioni 20 ni sawa tu ili kuwafanya vijana wanaotaka umaridadi waweze kuchangia serikali.”

Aidha Mbunge huyo ameipongeza serikali kwa bajeti nzuri ambayo amesema imegusa maisha ya watu wa chini kwa kujali miradi ya barabara, reli, ndege na bandari.

Source: Mtembezi
ZeroDegree.
Mbunge aunga mkono hatua ya serikali kuongeza kodi kwa wanaoandika majina yao kwenye magari, ataka kodi iwe milioni 20. Mbunge aunga mkono hatua ya serikali kuongeza kodi kwa wanaoandika majina yao kwenye magari,  ataka kodi iwe milioni 20. Reviewed by Zero Degree on 6/10/2016 09:23:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.