Loading...

Madereva wawili wafungwa miezi 6 jela kwa kutumia njia za magari ya mwendokasi.


MADEREVA wawili wa bodaboda wamefungwa jela miezi sita kwa kuendesha vyombo vya moto katika barabara ya mabasi yaendayo haraka jijini hapa.

Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, alitoa taarifa hiyo jana na kusema kuanzia sasa dereva atakayekamatwa akipita katika barabara hizo, hatatozwa faini bali atapelekwa mahabusu bila kupewa dhamana akisubiri kesi yake kufikishwa mahakamani.

Aliwataja madereva wa bodaboda waliofungwa miezi sita ni Hassan Mohamed (30) mkazi wa Tegeta aliyetiwa hatiani akiendesha pikipiki namba MC 299ABS aina ya SANLG kwenye barabara hizo maalumu.

Mwingine ni Rashid Sheha (45) mkazi wa Kimara aliyekuwa akiendesha pikipiki namba MC 379 ASV aina ya BOXER. Alisema katika operesheni hiyo iliyofanyika kuanzia Juni Mosi hadi Juni 6 mwaka huu kwenye wilaya za kipolisi za Kinondoni na Ilala, kati ya madereva 54 waliokamatwa, bodaboda ni 48 na sita ni wa magari binafsi.

Mpinga aliwataka madereva kuacha kupita katika njia hizo akisisitiza kwamba, hakutakuwa na faini bali wote watakaokamatwa watapelekwa mahabusu wakati utaratibu wa kuwafikisha mahakamani unafanyika.

“Watapigwa picha wakiwa wameshikilia kibao kinachoonesha majina yao, makabila, maeneo wanayotoka na waliyokamatwa, kazi zao, kosa walilotenda, tarehe na muda waliotenda kosa na kisha picha kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii,” alisema Mpinga.

Mpinga alisema tangu mabasi hayo yaanze kutoa huduma rasmi, Mei 10 mwaka huu hadi kufikia Juni 6, mwaka huu, zimetokea ajali 14 zikihusisha mabasi ya mwendo haraka na magari binafsi, pikipiki na bajaj.


ZeroDegree.
Madereva wawili wafungwa miezi 6 jela kwa kutumia njia za magari ya mwendokasi. Madereva wawili wafungwa miezi 6 jela kwa kutumia njia za magari ya mwendokasi. Reviewed by Zero Degree on 6/10/2016 09:31:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.