Loading...

Noti bandia zasambaa nchi nzima, Benki Kuu [ BoT ] yawataka wananchi kuwa makini ili kuepuka hasara..


Mfano wa noti bandia.

Mbeya. Meneja Msaidizi Kitengo cha Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Gloria Mwaikambo ametoa rai kwa wananchi kuwa makini na fedha bandia ili kuepuka hasara.

Mwaikambo amesema tatizo la noti bandia limekuwa kubwa nchini, kwani wananchi wengi hawajui jinsi ya kuzitambua.

Mwaikambo amesema hayo jana mjini Mbeya kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo.

Amesema tatizo hilo limeenea nchi nzima, hivyo amewataka wananchi watambue alama 11 za kutambua fedha halali na bandia.

Wakati huo huo, Katibu Tawala Wilaya ya Kyela, Geofrey Anania ameishauri BoT kuhakikisha inaimarisha thamani ya shilingi ili kuleta ushindani kwenye Soko la Kimataifa, tofauti na sasa inaonekana kuzidiwa na fedha za kigeni.


ZeroDegree.
Noti bandia zasambaa nchi nzima, Benki Kuu [ BoT ] yawataka wananchi kuwa makini ili kuepuka hasara.. Noti bandia zasambaa nchi nzima, Benki Kuu [ BoT ] yawataka wananchi kuwa makini ili kuepuka hasara.. Reviewed by Zero Degree on 6/24/2016 11:42:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.