Loading...

Mkazi wa Dodoma, ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na nyara za Serikali kinyume cha sheria.


Babati. Mkazi wa Kijiji cha Getakulu wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma, Kidua Mafyeko (34) amehukumiwa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na nyara za Serikali kinyume cha sheria.

Akisoma hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi wa Mahakam ya Mkoa wa Manyara, Bernard Nganga alisema vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani ni ushahidi usio na shaka kwamba, mshtakiwa alikuwa akijihusisha na ujangili.

Hakimu Nganga alitaja nyara hizo na thamani yake kuwa ni pembe mbili za kongoni, mkia wa nyumbu, ngozi ya pundamilia vyenye thamani ya Sh5.3 milioni.

Awali, Wakili wa Serikali, Timotheo Mmari, Mwendesha Mashtaka wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Linus Bugaba na Joachim Msemo wa Polisi, waliiomba Mahakama hiyo itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa majangili wengine.


ZeroDegree.
Mkazi wa Dodoma, ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na nyara za Serikali kinyume cha sheria. Mkazi wa Dodoma, ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na nyara za Serikali kinyume cha sheria. Reviewed by Zero Degree on 6/24/2016 11:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.