Serikali YATOA MSIMAMO wake juu ya suala la MAPENZI ya Jinsia moja.
Alisema hayo jana wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa haki za binadamu uliofanyika Dar es Salaam, kujadili mapendekezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu na kuweka mikakati ya kuishawishi serikali kukubali mapendekezo mengine ambayo iliyakataa.
Mpanju ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, alisema mapendekezo yaliyowasilishwa Mei mwaka huu katika mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu uliofanyika Geneva, alisema serikali ilikubali mapendekezo 130 na mengine 72 iliyakataa.
“Sehemu ya mapendekezo hayo serikali iliyakataa kwa sababu kuna mengine yapo kinyume cha Katiba, sheria, mila na desturi zetu, kwani katika mapendekezo hayo yapo yanayotaka mapenzi ya jinsia moja, jambo ambalo haliwezi kukubalika,” alisema Mpanju.
“Hivyo wakati mkijadili namna ya kupanga mikakati ya utekelezaji ili serikali ione umuhimu wa kukubali sehemu ya mapendekezo hayo naomba msijielekeze kwenye yale yaliyo kinyume na imani,” alisisitiza Mpanju.
Source: Mtembezi
ZeroDegree.
Serikali YATOA MSIMAMO wake juu ya suala la MAPENZI ya Jinsia moja.
Reviewed by Zero Degree
on
6/29/2016 02:55:00 PM
Rating: