Loading...

Simu zote feki kufungiwa kesho.


WAKATI kesho Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikitarajiwa kutimiza azma yake ya kuzima simu ‘feki’ za mkononi, upo mtikisiko na kizaazaa miongoni mwa watumiaji wa vifaa hivyo vya mawasiliano, wakisaka mbadala na wengine wakisubiri kuona kama ‘yatatimia’.

Ingawa uzimaji wa simu bandia na kuanza kutumika kwa teknolojia mpya ya simu za mkononi kwa Mfumo wa Rajisi, unatarajiwa kuwa muarobaini wa wizi kwa simu za mkononi na kiama kwa watukanaji, watumaji picha chafu, baadhi ya wanajamii wanaipokea hatua hiyo kwa mtazamo hasi, wakiangalia hasara watakayopata baada ya simu zao kufungiwa.

Kizaazaa kimekumba siyo tu watumiaji wa simu, hususan wale ambao wameshabaini kuwa simu zao ni bandia, bali pia wenye maduka ya simu ambao baadhi inadaiwa kusafirisha simu hizo kwenda kuziuza nchi jirani.

Wakati hayo yakijiri miongoni mwa watumiaji wa simu za mkononi, kwa upande wao, kampuni za simu za mkononi zimetumia fursa hiyo kufanya biashara ya simu za mkononi kwa bei nafuu, itakayowezesha wenye kipato cha chini kumudu bei yake.


ZeroDegree.
Simu zote feki kufungiwa kesho. Simu zote feki kufungiwa kesho. Reviewed by Zero Degree on 6/15/2016 10:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.