Loading...

Utapiamlo waishtua Serikali


Dar es Salaam. Utapiamlo na udumavu wa akili vinaonekana kushtua Serikali na kuamua kuondoa kodi kwenye vitamini, virutubishi na dawa za kusafisha maji ukiwa ni mkakati wa kuimarisha afya za wananchi.

Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 42 ya watoto chini ya miaka mitano wamedumaa, wakati asilimia 16 walipoteza maisha na 21 ya watoto walizaliwa wakiwa na uzito wa chini.

Akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2016/17 jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema Serikali imetenga asilimia 9.2 ya bajeti yake yote kwa ajili ya afya, wakati elimu imepangiwa asilimia 22.1 kuwezesha kuboresha sekta hiyo inayohusisha utoaji elimu bure kuanzia msingi hadi kidato cha nne.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Utapiamlo waishtua Serikali Utapiamlo waishtua Serikali Reviewed by Zero Degree on 6/09/2016 04:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.