Loading...

Vardy afuzu vipimo Arsenal.


Jamie Vardy.

Kocha Mkuu wa klabu ya Arsenal maarufu kama washika bunduki wa jiji la London Mfaransa Arsene Wenger ameanza kukimega kikosi cha mabingwa wa ligi kuu ya England EPL Leicester City akistukiza usajili wa mshambuliaji hatari wa timu hiyo Jamie Vardy.

Klabu ya Arsenal inaharakisha ukamilisho wa dili la usajili wa kustukiza pauni milioni 20 kwa mshambuliaji hatari wa Leicester City Jamie Vardy kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro 2016.


Washika bunduki hao wa kaskazini mwa London Arsenal wamefikia thamani ya mauzo ya mchezaji huyo na wanamatumaini ya kukamilisha dili hiyo ndani ya masaa 24 kabla ya kikosi cha timu ya taifa ya England hakijaelekea nchini Ufaransa kwenye michuano ya Euro 2016.

Katika mkataba ujao Arsenal wameahidi kumwongezea mshahara zaidi kwa juma kuliko anaolipwa sasa wa pauni elfu 80.


Jamie Vardy anataraji kueleka nchini Ufaransa kesho jumatatu akiwa tayari ni mchezaji mpya wa Arsenal baaada ya kukamilisha uhamisho huo wa pauni milioni 20 kutoka Leicester City.


ZeroDegree.
Vardy afuzu vipimo Arsenal. Vardy afuzu vipimo Arsenal. Reviewed by Zero Degree on 6/06/2016 10:23:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.