Loading...

Wabunge UPINZANI HATARINI Kufutiwa posho kwa kitendo cha kususa vikao vya Bunge.


WABUNGE wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambao wamekuwa wakiingia bungeni kusaini posho na kuondoka, wako hatarini kufutiwa posho kama wataendelea kususa vikao vya Bunge kama walivyotangaza.

Hali hiyo inatokana na hoja zaidi ya mbili zilizowasilishwa kwa Spika wa Bunge kwa njia ya Mwongozo huku moja ikiwasilishwa na Waziri mwenye dhamana ya Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe, zikikusudia kutaka Bunge kufuta posho za wabunge hao.

Akizungumza jana bungeni baada ya kuruhusiwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, Dk Mwakyembe akitumia ibara za Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na Kanuni za Kudumu za Bunge, alitaka uongozi wa Bunge kutazama upya kama wabunge hao wanastahili kulipwa posho.

Dk Mwakyembe, kwanza alitumia Ibara ya 26 ibara ndogo ya kwanza na ibara ndogo ya pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo aliinukuu; “Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano. 
Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria za nchi.”

Baada ya hapo alinukuu tena Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 23, ibara ndogo ya kwanza na ya pili; “Kila mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote, anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo kulingana na kiasi na sifa za kazi wanayoifanya. Kila mtu anayefanya kazi anastahili kupata malipo ya haki.”

Kwa kuzingatia ibara hizo za Katiba, alisema kwa kutumia nafasi yake ya raia wa Tanzania na Waziri mwenye dhamana ya Katiba na Sheria, alihoji kama haki inatendeka, kulipa posho na stahiki wabunge ambao hawakuingia bungeni wala hawakuwa katika shughuli inayotambuliwa na Bunge, sawa na waliokuwa wakifanya kazi bungeni.





ZeroDegree.
Wabunge UPINZANI HATARINI Kufutiwa posho kwa kitendo cha kususa vikao vya Bunge. Wabunge UPINZANI HATARINI Kufutiwa posho kwa kitendo cha kususa vikao vya Bunge. Reviewed by Zero Degree on 6/03/2016 08:23:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.