Loading...

Wabunge wajitoa KAMATI YA UKIMWI baada ya kukataliwa safari ya Marekani.


WABUNGE wa Kambi ya Upinzani Bungeni walio katika Kamati ya Ukimwi wametangaza kujitoa kwenye kamati hiyo kwa maelezo ya kukataliwa safari ya Marekani kuhudhuria mkutano kuhusu masuala ya Ukimwi.


Mwita Waitara

Mjumbe wa kamati hiyo, ambaye ni Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara, aliwaeleza wanahabari bungeni mjini hapa juzi kuwa, waliteuliwa wajumbe watatu kuhudhuria mkutano huo wa siku tatu kuanzia Juni 8, mwaka huu huko New York, Marekani, lakini baadaye aliruhusiwa mjumbe mmoja wa CCM.

Kwa mujibu wa Waitara, walioteuliwa na Spika kwenda kwenye mkutano huo ni yeye (Waitara), Mbunge wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu (CCM) na Mwenyekiti wa Wanawake (CUF) ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu, Severine Mwijage waliokuwa wamekwishapata Viza.

Alisema, “safari yetu ilisitishwa kwa simu bila kuelezwa sababu na akaachwa Mwenyekiti wa Kamati yetu ambaye ni Mbunge wa CCM. Kutokana na hilo, tunajitoa kwenye kamati ya Ukimwi.”

Naibu Katibu wa Bunge, John Joel amethibitisha kutenguliwa kwa majina ya wabunge wawili wa upinzani katika safari hiyo ya Marekani na kusema aliyewateua ambaye ni Spika wa Bunge ndiye aliyewatengua kwa sababu za msingi.

Aliongeza kuwa, suala hilo halina uhusiano wowote na Rais John Magufuli anayemtuhumu kuweka shinikizo la kuwaondoa katila orodha ya safari hiyo.

Source: Mtembezi
ZeroDegree.
Wabunge wajitoa KAMATI YA UKIMWI baada ya kukataliwa safari ya Marekani. Wabunge wajitoa KAMATI YA UKIMWI baada ya kukataliwa safari ya Marekani. Reviewed by Zero Degree on 6/12/2016 10:19:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.