Loading...

Watu 36 wauawa katika shambulio la kujitoa muhanga nchini Uturuki.


Watu 36 wameuawa katika shambulio la kujitoa muhanga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ataturk Istanbul nchini Uturuki,na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa.

Shughuli za usafirishaji katika uwanja huo zimesitishwa huku shughuli ya uokoaji na huduma ya kwanza vikiendelea..

Gavana wa mji wa Istanbul amethibisha kuuawa watu hao 32 na idadi hiyo ya majeruhi.



Lango la uwanja wa ndege.

Mashuhuda wanasema waliwaona washambuliaji watatu,ambapo mmoja kati yao alikuwa akifyatua risasi kabla ya kujitoa muhanga kwa kujilipua kwa bomu na kufa.

Hata hivyo mashambulizi hayo yalihusisha katika eneo la kuingia katika uwanja huo.

Rais wa Uturuk Recep Tayyip Erdogan amelaani shambulio hilo na kusisitiza umoja katika kutokomeza vitendo hivyo.

Uturuki imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya kigaidi kutoka pande mbili,kwanza kutoka kwa kundi la Islamic State wanaoingia kutoka nchi jirani ya Syria na waasi wa Kikurud wanataka kuunda dola yao.


Source: BBC
ZeroDegree.
Watu 36 wauawa katika shambulio la kujitoa muhanga nchini Uturuki. Watu 36 wauawa katika shambulio la kujitoa muhanga nchini Uturuki. Reviewed by Zero Degree on 6/29/2016 10:33:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.