Loading...

Hifadhi ya gesi ya Helium ya futi za ujazo Bilioni 54 yagunduliwa Tanzania.


GESI ya helium ya takribani futi za ujazo bilioni 54 inayoelezwa kuwa adimu duniani, imegundulika nchini Tanzania na kuiweka nchi kuwa miongoni mwa mataifa machache yenye madini mengi na muhimu.

Wagunduzi wa gesi hiyo ni watafiti kutoka vyuo vikuu viwili nchini Uingereza vya Oxford na Durham kwa kushirikiana na wataalamu wa madini kutoka nchini Norway.

Watafiti hao wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi hiyo ya barafu, kama inavyofahamika katika eneo la Bonde la Ufa nchini.

Taarifa za waandishi wa habari nchini Japan, zimeeleza kuwa watafiti hao wamesema kuwa uhaba wa gesi hiyo duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari, ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama ‘MRI scanners’.

Pia hutumia katika mitambo ya kinyuklia na katika sekta nyingine nyingi za kiteknolojia.


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Wiki iliyopita, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati akijibu swali bungeni mjini Dodoma alisema madini yanayotumika kwa ajili ya mitambo ya Apollo na pia vifaa vya matibabu kama MRI na NMR, yamegundulika kuwepo nchini Tanzania.

Hata hivyo, hakufafanua zaidi kiasi cha madini hayo na namna nchi itakavyonufaika na ugunduzi huo. Hata alipotafutwa jana, simu yake ya mkononi ilipokewa na msaidizi wake na kueleza kuwa waziri yuko kikaoni. Madini aina ya helium yanatumika kwa ajili ya mitambo na pia kwenye vifaa vya matibabu kama MRI na NMR.

Kabla ugunduzi huo, watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo ifikapo mwaka wa 2035.


Wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.

Mnamo mwaka 2010, mwanasayansi ambaye alikuwa mshindi ya Tuzo la Nobel, Robert Richardson alitabiri kumalizika kwa gesi hiyo katika kipindi kifupi. Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu, kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura.

Mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, Chris Ballentine alisema gesi hiyo iliyopatikana nchini inaweza kujaza silinda za gesi milioni 1.2 za mashine za MRI.


ZeroDegree.
Hifadhi ya gesi ya Helium ya futi za ujazo Bilioni 54 yagunduliwa Tanzania. Hifadhi ya gesi ya Helium ya futi za ujazo Bilioni 54 yagunduliwa Tanzania. Reviewed by Zero Degree on 6/29/2016 10:43:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.