Loading...

15 wauawa katika shambulizi la kigaidi Baghdad.

Walinda usalama pamoja na wafanyikazi wa kimatibabu mjini Baghdad, wanasema kuwa yamkini watu 15 wameuwawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa, baada ya mlipuaji wa kujitoa muhanga kujililipua katika mji huo mkuu wa Iraq.

Mlipuaji huo alilipua vilipuzi katika eneo la kiusalama langoni mwa kuingia katika Wilaya ya Kadhimiyah, kuliko na waislamu wengi wa Ki-Shia.

Makundi ya walinda usalama kwa sasa wamezingira eneo hilo na kudumisha ulinzi mkali katika maeneo yote ya vituo vya kiuslama kote mjini Baghdad.

Hakuna kundi lolote ambalo limekiri kutekeleza shambulio hilo.


Credits: BBC
ZeroDegree.
15 wauawa katika shambulizi la kigaidi Baghdad. 15 wauawa katika shambulizi la kigaidi Baghdad. Reviewed by Zero Degree on 7/24/2016 01:52:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.