Loading...

PESA INAONGEA: Gonzalo Higuain atua Juventus akitokea Napoli kwa dolla milioni 103.

Ni usajili mukubwa ambao ulioleta gumzo mitandaoni, huku wengi wakichukulia kama moja ya uhamisho wa gharama katika historia ya soka.

kulingana na Sky Sports, Juventus wamemsajili Gonzalo Higuain kutoka Napoli kwa dolla za kimarekani 103, huo utakua uhamisho wa pili wa gharama kubwa kutokea katika historia ya soka duniani (Cristiano Ronaldo).

Usajili wa Higuain(28), unaonekana kuwa gumzo kulingana na kiasi kikubwa cha pesa pamoja na kwamba ndiye straika anayeongoza Serie A kwa kufumania nyavu. Goli 36 ndani ya mechi 35 ilikua ni kama mkakati mkubwa na mgumu sana kwake, ingawa anabaki kuitwa mshambuliaji bora.

Kiasi hicho kikubwa cha pesa itakua kama mskumo kwa Juventus kumuuza Paul Pogba kwenda klabu ya Manchester United or Real Madrid kwa ada ya uhamisho itakayokua ya kwanza kutokea katika historia ya soka, karibia na dola milioni 110 ambazo Real Madrid walilipa kwa ajili ya Gareth Bale mwaka 2013.

Klabu ya soka ya Arsenal ni moja wapo kati ya waliokua wakifukuzia saini ya nyota huyo, lakini ikabaki kuwa ngumu kwao kulingana na kushindwa kuelewana katika malipo na vile vile mapenzi aliyonayo Arsene Wenger‘s ya kupenda kutumia wachezaji wenye umri mdogo.
Credits: NBC Sports.
ZeroDegree.
PESA INAONGEA: Gonzalo Higuain atua Juventus akitokea Napoli kwa dolla milioni 103. PESA INAONGEA: Gonzalo Higuain atua Juventus akitokea Napoli kwa dolla milioni 103. Reviewed by Zero Degree on 7/24/2016 01:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.